The House of Favourite Newspapers

Mchongo Mzima wa Mobetto na Ricky Ross

0

MAMA wa mwanamama staa wa fani nyingi nchini Tanzania, Hamisa Hassan Mobeto, Shufaa Rutiginga anasema kuwa, hata siku moja hawezi kumchagulia au kumpangia mtu wa kumuoa mtoto wake huyo baada ya kuwepo kwa tetesi juu ya mchongo mzima wa kuolewa na staa wa Hip Hop wa Marekani, William Leonard Roberts almaarufu Rick Ross.

 

Katika mahojiano na mtangazaji Lil Ommy wa Tanzania, Rick Ross alithibitisha kuwa na koneksheni na Mobeto, lakini akasisitiza kwamba, mwenye uwezo wa kuzungumzia koneksheni hiyo ni mwanamama huyo.

 

“Lazima niseme ukweli, kuna uhusiano, ni kiasi gani unataka nitakuambia juu yake? Nitamwachia yeye…lakini yeye ni mtu mzuri sana, mrembo roho na yeye ni mjasiriamali mkubwa na ninataka kumsaidia kuipeleka katika kiwango kingine kwa sababu anafanya kazi nzuri na ninajivunia.

 

“Kuna mambo mengine kadhaa, lakini yote kwa yote nataka kumuona akishinda,” alisema Rick Ross akisisitiza ana mpango wa kutinga Tanzania hivi karibuni.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mama huyo anasema kuwa, anaona kwenye mitandao watu wengi wanamuuliza, vipi kuhusu mtoto wake kuolewa na Rick Ross; staa mkubwa wa muziki wa Marekani, kitu ambacho hawezi kukijibu kwa sababu ni maswali yanayomuhusu Mobeto mwenyewe.

 

“Ukweli ni kwamba mimi sina uamuzi wa kumchagulia Hamisa (Mobeto) mchumba wa kumuoa, kila kitu kiko mikononi mwake hivyo tumuachie mwenyewe na uamuzi wake,” anasema mama huyo.

 

Kwa upande wa Mobeto aliliambia IJUMAA kuwa, watu wengi wanamtabiria kuwa ataolewa na Rick Ross na mambo mengine kibao, lakini ukweli ni kwamba bado yupoyupo sana.

 

“Ukweli ni kwamba mimi bado niponipo sana sina mpango wa kuolewa leo au kesho kwa sababu, nina mambo yangu mengi sana ya kufanya kwa sasa hivyo hayo mambo ya mtandaoni ni ya kufikirika,” anasema Mobeto.

 

STORI; IMELDA MTEMA, BONGO

Leave A Reply