The House of Favourite Newspapers

Penzi la Jux, Huddah Limekaa Hivi

0

MSANII anayefanya poa kunako anga la Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’, amefungukia tetesi za kutoka kimapenzi na mrembo maarufu mitandaoni wa Kenya, Huddah.

 

Jux anasema kuwa, ukaribu wao siyo wa kimapenzi, bali ni wa kikazi na muda siyo mrefu mashabiki wao wataona kitu kikubwa kutoka kwao.

 

Madai ya wawili hao kuwa wapenzi yaliibuka mara baada ya kuonekana visiwani Zanzibar wakiwa pamoja.

 

Akizungumza na IJUMAA SHOWBIZ, Jux anasema kuwa, ni kweli walikuwa katika hoteli moja, lakini hakuna lolote lilotokea kati yao, lakini mashabiki wao wataona ni kitu gani hasa walikuwa wanafanya Zanzibar.

 

“Ni kweli tulikuwa Zanzibar, lakini hatukuwa na ukaribu huo, kuna kazi tulikuwa tunafanya hivyo itakapokuwa tayari watu wataona,” anasema Jux ambaye hivi karibuni alipitia changamoto ya maneno mengi baada ya aliyekuwa mwandani wake, Vanessa Mdee kuanika ujauzito wake kwa mpenzi wake wa sasa, Rotimi.

 

STORI: KHADIJA BAKARI

Leave A Reply