The House of Favourite Newspapers

Exclusive: Meneja Atoboa Siri ya Harmo Nigeria

0

UNAAMBIWA katika maisha ili ufanikiwe, basi ni lazima kuwe na ushindani, iwe wa kikazi au kibiashara.

Baada ya staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kukwea pipa kwenda nchini Afrika Kusini (Sauzi) kwa ajili ya kurekodi album yake mpya huku nyuma mpinzani wake, Rajab Abdul ‘Harmonize’ naye bila kuchelewa amekimbilia nchini Nigeria kujibu mapigo.

Vyanzo vya karibu vimeliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, Harmonize au Harmo yupo nchini Nigeria kwa ajili ya maandalizi ya album yake mpya.

 

Katika safari hiyo, Harmo ameambatana na wasanii wake wa Lebo ya Konde Gang, Ibraah na Country Wizzy.

Wakiwa nchini Nigeria, walipata mapokezi mazuri kutoka kwa memba wao mwingine ambaye ni mwanamuziki wa Nigeria aitwaye Skales.

 

Ili kupata kinaubaga kilichowapeleka nchini humo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limefanya mahojiano maalum (exclusive interview) na mmoja wa mameneja wa Harmo aitwaye Rajab Mchopa ambaye ametoboa siri ya kilichowapeleka nchini humo.

IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Mchopa?

MCHOPA: Poapoa niambie…

IJUMAA WIKIENDA: Asante, hivi Nigeria mmekwenda kufanya nini? Maana tunasikia tu tetesi mitandaoni kwamba mmeenda kurekodi album?

 

MCHOPA: Ni kweli huku Nigeria tumekuja kwa ajili ya kurekodi album mpya ya Harmonize hivyo mashabiki wa Harmo wakae mkao wa kula, najua hawatamuangusha msanii wao kipenzi, lakini pia wasisahau kuwa siyo Harmo tu hata Ibraah na Country Boy pia wamekuja huku kwa ajili ya kumalizia album zao.

IJUMAA WIKIENDA: Mnatarajia kukaa huko kwa muda gani?

 

MCHOPA: Nadhani tutakaa huku kwa muda wa wiki mbili mpaka tatu hivi.

IJUMAA WIKIENDA: Kuna baadhi ya watu wanadai eti mmemuiga aliyekuwa bosi wa Harmo, Diamond Platnumz ambaye yeye amejichimbia zake nchini Afrika Kusini, hii imekaaje?

 

MCHOPA: Siyo kweli, muda wa sisi kwenda Nigeria ulikuwa umeshafika kwa sababu ni safari ambayo tuliipanga muda mrefu sana.

IJUMAA WIKIENDA: Album inaitwaje na itakuwa na ngoma ngapi?

 

MCHOPA: Kitu ambacho watu wanatakiwa wakifahamu kwa sasa ni kwamba album inaitwa High School, kuhusu kolabo na listi ya nyimbo zitakazokuwepo naomba waendelee kusubiri mpaka pale tutakapoitangaza rasmi.

IJUMAA WIKIENDA: Tutegemee kuona mastaa gani wakubwa kutoka nje ya Tanzania kwenye albam hiyo?

MCHOPA: Surprise ni nyingi sana hivyo naomba mashabiki waendelee kuwa wapole, lakini zaidi wasiache kuendelea kuisapoti ngoma mpya ya Attitude ambayo bado inashika namba moja (Youtube).

 

Harmo anaungana na mastaa wengine wa Bongo ambao wamekwenda nje kuandaa albam zao kama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Faustina Charles ‘Nandy’ na wengine kibao.

Hii itakuwa ni albam ya pili kwa Harmo baada ya ile aliyoiachia mwaka jana ya Afro East.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply