The House of Favourite Newspapers

Mke wa King Kiki Azungumzia Afya ya Mumewe

0

CONSTANSIA Kalanda ambaye ni mke wa msanii muziki wa dansi nchini Tanzania, King Kiki, amefunguka kuhusu kuumwa kwa mumewe huyo huku akiwaonya wanaochukua jukumu la kuzungumzia afya ya mumewe.

 

King Kiki ni mmiliki wa bendi ya La Capital, inayotesa na mtindo wake wa Kitambaa Cheupe. Habari za kuumwa kwa King Kiki zilizagaa wiki iliyopita zikimuonyesha akiwa katika picha na familia yake kitandani wakimpa msaada wa kukaa.

 

Taarifa hizo zilisema, “Anaumwa yuko kitandani  anahitaji msaada wa hali na mali. Alikuwa anaumwa mgongo na baadaye kupooza, alilazwa Muhimbili gharama zikawa kubwa sasa anaugulia nyumbani kwake.”

 

Akizungumzia jambo hilo,  Costansia, amesema taarifa za kuwa mume wake anaumwa ni za kweli japokuwa amekanusha kuwa familia haijashindwa kumhudumia kimatibabu.

 

“Ni kweli King Kiki anaumwa, lakini taarifa kuwa ametoka hospitali kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu hazina ukweli wowote kwani familia tupo tunamhudumia,” amesema.

 

Akizungumzia kuhusu ugonjwa unamsumbua,  amesema alipata tatizo la uti wa mgongo kama mwezi mmoja uliopita na kufanyiwa upasuaji wa pingili za shingo wiki mbili zilizopita.

 

Amesema kutokana na upasuaji huo alijikuta akishindwa kunyanyuka na kukaa mwenyewe kutokana na madhara aliyopata wakati wa kuwekewa ganzi.

 

“Madaktari wametumbia kwa kuwa kutokana na  Kiki kuwa mtu mtu mzima ilibidi wampige ganzi ile ya kuuwa mwili mzima wakati wa kumfanyia upasuaji.

 

“Ni kutokana na hilo walisema ingemchukua takribani wiki mbili kurudi katika hali yake ya kawaida na mpaka tunafika leo wiki mbili hizo tayari zimefika, hapa tunafanya utaratibu kesho tumrudishe hospitali kwa uchunguzi zaidi,” amesema.

 

Hata hivyo, amewaonya watu wanaojitwika usemaji wa familia kwa kumzungumzia msanii huyo na kusema kwamba wanaopaswa kufanya hivyo ni yeye na mtoto wake mkubwa wa kiume.

 

Pia aliwaondoa hofu mashabiki wa msanii huyo na kueleza kuwa hayupo katika hali mbaya kihivyo kama inavyosemwa, huku akiwaomba wamuombee ili aweze kunyanyuka na kuendelea na kazi zake za sanaa.

Leave A Reply