The House of Favourite Newspapers

Msikubali Kutapeliwa Kupitia Kajala

BAADA ya watu mbalimbali kuibuka na kudai kuwa wametapeliwa na mtu anayejiita Kajala kwenye mitandao ya kijamii, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ amesema watu wasikubali kuingizwa mkenge.

 

Kajala ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa ameamua kusema hili kwa sababu ameonekana wazi hivyo akikaa kimya ipo siku atabebwa msobemsobe na kupelekwa polisi kwa kosa la wajanja wa mjini.

 

“Hakuna kitu ambacho sikipendi kama mtu kutumia jina langu kwa utapeli, yaani inakera sana maana ipo siku nitajikuta nalala polisi, kisa nadaiwa nimechukua pesa ya mtu tena kwa njia ya mtandao. Kwa hiyo ninawasihi watu wawe makini, sina akaunti Facebook na siwezi kumuomba mtu pesa,” alisema Kajala.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.