The House of Favourite Newspapers

Odemba Hata Haoni Aibu!

WAKATI wengine wakijivalisha digirii kutokana na umaarufu walio nao kwenye jamii, mwanamitindo Miriam Odemba amevunja ukimya na kusema kuwa haoni aibu kusema ameishia darasa la saba.

 

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Odemba alisema watu wengine wanaona aibu kusema kuwa hawajasoma kwa sababu wanataka kujionesha kwa watu, lakini kwa upande wake ameishia darasa la saba na hawezi kulificha hilo.

 

“Kwa nini nijikweze nimesoma wakati nimeishia darasa la saba halafu baadaye ndiyo nikajiendeleza, lakini sekondari sikuiona na nilitamani sana nipate elimu hiyo na hata nikiona wanafunzi wamevaa sare za sekondari natamani miaka irudi nyuma,” alisema Odemba.

Comments are closed.