The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Wa Kidato Cha 4 Atuhumiwa Kuchoma Moto Madarasa Mawili Mbeya

0
Kamanda wa Polisi-Mbeya, Benjamin Kuzaga

Mwanafunzi Yesse Charles mwenye umri wa miaka 17 anatuhumiwa kufanya tukio hilo katika Shule ya Sekondari ya Serikali Iyela kwa kutumia mabua na karatasi kuanzisha moto huo na kuteketeza vyumba viwili vya madarasa, nguo, magodoro na madaftari ya Wanafunzi
Kamanda wa Polisi-Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema chanzo cha tukio ni chuki ya Mwanafunzi baada ya kuadhibiwa na Mkuu wa Shule kwa kosa la utovu wa nidhamu
Afisa Elimu Mbeya (Sekondari), Ernest Hinju amesema “Shule ya Iyela ilikuwa na ufaulu mbovu wa Kidato cha Nne, Mwaka 2021 waliopata daraja 0 ni 147, tukafanya mabadiliko ya uongozi, Mwaka 2022 waliopata daraja 0 ni 29. Wakati tunapambana kuiweka Shule sawa Mwanafunzi anachoma moto madarasa, ametukosea na atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria”

Leave A Reply