The House of Favourite Newspapers

Mwizi Aogeshwa Maji ya Tope, Akimbia Kipigo Kutoka kwa Wananchi, Polisi Wamuokoa

0
Mwizi akiogeshwa maji machafu pamoja na tope

KIJANA ambaye hajafahamika haraka jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30 mkazi wa Igoma halmashauri ya mji wa Njombe amenusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage mara baada ya kukamatwa akiwa ameiba vitu mbali mbali Ikiwemo TV,Godoro,Blanketi na Mtungi mdogo wa gesi.

 

Luo Lameck Mgeni ni mzee aliyekuwa amempangisha awali katika nyumba yake kabla ya kumfukuza kutokana na tabia ya wizi anasema anashangaa kuona kijana huyo ameondoka kwake lakini amerudi na kuiba kwenye moja ya nyumba ya familia yake.

Mwizi akiwa amewekwa chini ya uangalizi mjini Njombe

“Leo nikasikia kule nyumbani wameboboa nikauliza wameiba nini,kuingia mle ndani tukaona tandiko halipo na vitu vingine amechana chana ameweka nje”alisema Mzee Mgeni

 

Hata hivyo kabla kijana huyo hajafikiwa na hali mbaya kutokana na kipigo,Polisi wamefika na kufanikiwa kumuondosha katika eneo hilo.

Leave A Reply