visa

NANDY: BILLNAS ALINIPA DAWA NIKAMEZA, MIMBA IKATOKA

MSANII wa kike anayefanya vizuri kwenye game ya muziki wa Bongo Fleva, Nandy a.k.a African Princess, ameanika siri ambayo watu wengi walikuwa hawaifahamu kuhusu kushika ujauzito wa msanii mwenzie, Billnas ambaye waliwahi kuwa wapenzi.

 

Akipiga stori na kituo kimoja cha redio nchini, Nandy ambaye hivi karibuni ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao BUGANA alioimba na Billnas, anasema wakati wakiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi aliwahi kushika ujauzito na Billnas, lakini kwa bahati mbaya ‘ULITOKA’.

 

Amesema hiyo ilikuwa ni baada ya Billnas kumletea dawa ambazo hakujua kama zingesababisha ujauzito ule utoke. “Nilikuwa excited sana na ujauzito ule na niliumia sana ulipotoka lakini sikuwa na jinsi maana ilishatokea na sitaki kukumbuka tena..,” alisema Nandy.
Toa comment