The House of Favourite Newspapers

Nandy Hakamatiki Afrika Mashariki, Shuhudia Alichokifanya

0

 

MWANADADA anayepeperusha bendera ya Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ameendelea kuwafunika mastaa wa kiume wa muziki huo nchini huku akizidi kupasua anga katika ukanda wa kimataifa hususan Afrika Mashariki.

 

Kwa uwezo wake wa kutengeneza muziki mzuri, katika kipindi cha mwaka huu Nandy amefanikiwa kupenya kwa kufanya kolabo na wasanii wakubwa na sasa anawapanga tu kwenye foleni kimafanikio.

 

Baadhi ya wasanii wanaotajwa kuachwa mbali na Nandy katika mafanikio ya kimuziki mwaka huu ni pamoja na Ali Saleh ‘Alikiba’, Juma Jux, Elias Barnabas ‘Barnaba boy’, Mbwana Kilungi ‘Mboso’, Abdul Iddi ‘Lavalava’, Raymond Mwakyusa ‘Rayvan’.

 

Nandy anabaki kuwa msanii mwanamke mahiri anayetajwa kuwa atafanya vizuri zaidi kwa miaka mingi ijayo ukilinganisha na umri alionao kwa sasa na mambo makubwa ambayo amefanya.

 

Tayari ana nyimbo nyingi kubwa na zenye rekodi ndani na nje ya nchi, kiasi cha kutwaa tuzo kubwa ya Msanii bora wa kike wa Afrika Mashariki na sasa anaisaka rekodi ya Afrika nzima.

 

Katika mahojiano maalumu RISASI kuhusu mafanikio yake kwa mwaka 2020, Nandy alisema anaamini kwamba, yeye ndiye msanii wa kike aliyefanya vizuri zaidi kuliko hata baadhi ya wasanii wa kiume.

 

Alitolea mfano kuwa nyimbo zake ‘zimetrendi’ kwenye chati mbalimbali za muziki ndani na nje ya Bongo.

Hata hivyo, Nandy alisema anahitaji kuendelea kupenya kwa kufanya kolabo na mastaa wakubwa wa muziki barani Afrika.

 

Pamoja na kwamba hakutaka kuweka wazi majina ya wasanii hao, lakini RISASI Jumamosi linafahamu kwamba Nandy yupo kwenye mipango ya kolabo na WizKid na Yemi Alade wa Nigeria na Tanasha Donna wa Kenya.

 

Nandy anajivunia mafanikio yake kwa mwaka 2020 kwa kufanikisha kutoa nyimbo tano ambazo ni Na Nusu, Acha Lizame akiwa na Harmonize au Harmo.

 

Nyingine ni Dozi, Do Me akiwa na mchumba’ke, William Lymo ‘Billnass’ kisha akamalizia na Nibakishie akiwa na King Kiba na nyimbo zote hizo zimefanya vizuri kwenye chati za muziki.

 

“Ukweli ni kwamba namba huwa hazidanganyi. Kwa mfano video ya Wimbo wa Na Nusu ina watazamaji milioni mbili, Acha Lizame ina milioni sita, Dozi ina milioni moja na Do Me ina milioni moja,” anasema Nandy.

 

TUZO MBILI

Akizungumzia kutwaa tuzo mbili za Msanii Bora wa Kike wa Afrika Mashariki mwaka huu, Nandy anasema;

“Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu, ni jambo kubwa kwa kazi yako kutambulika kimataifa, ninapewa tuzo, ninajiona bora.”

 

ALBAM YA THE AFRICAN PRINCES

Akizungumzia mafanikio ya Albam yake ya The African Princes ambayo imetazamwa, kusikilizwa na kupakuliwa mara milioni saba kwenye Mtandao wa Boomplay na kuwafunika mastaa kibao Bongo hasa wa kiume, Nandy alisema;

“Nashukuru sana kwa kuwa miongoni mwa albam zilizofanya vizuri mno na nina mpango wa kuachia albam nyingine next year (mwaka ujao 2021).

 

“Kuhusu kulinganishwa katika muziki sioni kama kuna ubaya kwa sababu hii ni biashara, lazima kuwe na vitu kama hivyo ili biashara iwe nzuri, ni jukumu la mtu kuichukulia positive (chanya) kwa hiyo kwangu mimi naona kitu kizuri kwa sababu wanatusapoti wote kwa pamoja.”

 

Aidha, Nandy anawashukuru mashabiki wake ndani na nje ya Tanzania kwa namna walivyomsapoti kwa mwaka 2020 huku akiwaomba waendelee kufanya hivyo kwa mwaka 2021 kwani mambo mengi mazuri

Leave A Reply