The House of Favourite Newspapers

Nandy: Tupo Fiti, Majeruhi Wamerudi Dar, Shoo Kama Kawa Sumbawanga – Video

BAADA ya basi aina ya Coaster lililokuwa kwenye msafara wa Tamasha la msanii Nandy (Nandy Festival) linalotarajiwa kufanyika huko Sumbawanga, kupata ajali kwa kupinduka maeneo ya Mikumi, Morogoro, usiku wa kuamkia leo, msanii huyo amefunguka ilivyokuwa na hali halisi ya majeruhi.

 

 

Kupitia akaunty yake ya Instagram, Nandy ameweka video akisema: “Najua kuna taarifa ambazo zimesambaa mitandaoni kuhusu ajali, ni kweli ilitokea lakini niwatoe hofu. Kila mtu yupo salama.

“Gari iliyopata ajali ni ile ya pili ambayo ilikuwa imebeba madansa, bendi na viongozi, lakini tunamshukuru Mungu kwamba wote tupo salama. Kama mlivyoona gari ilivyo lakini hakuna mtu aliyeumia.

 

“Gari ya wasanii tayari tumeshafika Iringa, na tupo njiani tunakuja Sumbawanga, waliokuwa kwenye lile gari lililopata ajali tuliwatoa na baadhi yao wamerudi Dar kwa ajili ya matibabu.

“Msiwe na wasiwasi wakazi wa Sumbawanga tunakuja, ndugu jamaa na marafiki mliokuwa mkitupigia simu msiwe na wasiwasi, tulikuwa hatupatikani kwa sababu ya mtandao lakini tupo njiani, Sumbawanga tunakuja,” amesema Nandy.

 

Msafara huo ulikuwa na wasanii Juma Nature, Whozu, Stamina, Nandy, Barnaba, Roma, Billnass, Ice Boy na Willy Paul. 

 

Ni bahati njema hapakuwa na kifo chochote.

 

NANDY Afunguka Kuhusu Ajali “Majeruhi Wamerudi Dar”

Comments are closed.