The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Shilole Barazani

0

MPIGA picha maarufu wa mastaa mbalimbali Issa Juma ‘ Rommy 3D’ ambaye kwa sasa ndio mpiga picha binafsi wa mjasiriamali na msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘ Shilole’, amesema mwisho wa mwaka huu kitaeleweka kuhusu suala la yeye na msanii huyo kufunga ndoa.

 

Akizungumza na AMANI, Rommy alisema watu wengi wanatakiwa watambue kwamba yeye na Shilole ni watu wanaofahamiana kwa siku nyingi.

 

Alisema ni vigumu kufafanua uhusiano wao kwa sasa lakini amesisitiza kuwa ukweli utajulikana mwisho wa mwaka huu.

 

“Mimi naomba watu wawe na subira tu, ishu yote itakuwa wazi mwisho wa mwaka huu na ninaomba wazingatie kuwa mimi nipo singo na Shilole yupo singo hivyo wasiwaze sana” alisema Rommy D ambaye inadaiwa na yeye ndoa yake imeota mbawa baada habari za kutoka na msanii huyo kumfi kia mkewe.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Leave A Reply