The House of Favourite Newspapers

Ndugai: Riba Bodi ya Mikopo Inawaumiza Watoto wa Masikini

0


SPIKA Job Ndugai amesema mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imegeuka biashara akieleza riba inayodaiwa na Bodi ya Mikopo ni kubwa na watoto wa masikini ndiyo wanaoumia zaidi.

Amesema hayo wakati akiunga mkono hoja ya Mbunge Ramadhan Ihondo wa Singida Kaskazini ambaye alipendekeza kuondolewa kwa riba katika mikopo kwani serikali haiwasaidii vijana.

Ameongeza kwamba kudai mkopo na riba ni sawa na biashara na kwamba ni utaratibu ambao hauna tofauti na wanaokopa fedha za kununua magari.

Leave A Reply