The House of Favourite Newspapers

Nandy: Kolabo na Koffi Imekula Milioni 70

0

 

STORI zinazotrendi mtandaoni ni kuhusu African Princess, Nandy, ambaye ameweka wazi kuwa wimbo wake mpya aliofanya na msanii Koffi Olomide kutoka Congo DR, umemgharimu zaidi ya shilingi milioni 70.

 

 

Amesema hana shaka yoyote kuhusu gharama za wimbo hata kama asipompa faida ila anachoamini ni kwamba atakuwa ameacha alama kwenye muziki wake.

 

 

 

“Sijaongeza sifuri mbele ila kwa mtu muelewa anajua ilivyo, kuna kurekodi video ambayo si chini ya milioni 15 au 16, kumvalisha Koffi Olomide na watu wake, wachezaji, mimi mwenyewe, magari na hoteli zenye hadhi ya nyota tano zaidi ya milioni 70, hata kama faida ikichelewa naamini itakuwa imeniachia alama,” amesema Nandy.

Leave A Reply