The House of Favourite Newspapers

Ni Vita ya Funga Mwaka

0

MUZIKI mzuri hutengenezwa na ubunifu ambao unafanywa na wasanii kwa kufanya kazi nzuri. Kazi ambayo inaweza kuishi miaka mingi na kusikilizwa au kutazamwa na vizazi vingi vya baadaye. Baada ya Dunia na mataifa mengi kukumbwa na janga la Virusi vya Corona, mambo mengi yalisimama na bado yamesimama kwa baadhi ya mataifa duniani. Janga hili limeathiri maisha ya wengi.

 

Miongoni mwao ni wasanii ambapo wamejikuta hawawezi kufanya matamasha makubwa duniani kwani mikusanyiko haikuruhusiwa au hairuhusiwi na baadhi ya nchi anga kwa ajili ya ndege limefungwa. Kama ujuavyo, akili ya binadamu ha­ awahi kushindwa jambo hivyo wasanii wamejikuta wakigeuka na kutumia fursa nyingine mitandaoni.

 

Huku wamekuwa wakiachia ngoma zao na kutikisa vilivyo huku mkwanja ukizama kwenye akaunti zao za benki. Baadhi yao ni Harmonize, Kiba, Diamond, Zuchu, Nandy, Ibraah, Rayvanny, Mbosso, Jux na wengine wengi. Baadhi yao walifanya kolabo zilizotikisha vilivyo kwenye mitandao hiyo na sasa kinachoendelea ni vita kubwa ya kuufunga mwaka huu wa 2020.

 

Zikiwa zimesalia siku chache kwa mwaka kugeuka, baadhi ya wasanii wametangaza kukiwasha kwelikweli kama sehemu ya kuuaga mwaka wa 2020. Ifuatayo ni listi ya ngoma za kolabo ambazo zimetokea kubamba ipasavyo na nyingine zinakuja kwa ajili ya kuufunga mwaka huu kwa kishindo;

RAYVANNY NA ZUCHU (NUMBER ONE)

Gha‑ a tu, Number One kutoka kwa memba wa Lebo Wasa Classic Baby (WCB), Rayvanny na Zuchu imekamata vilivyo na kuendelea kuweka rekodi zake za kila aina huko mitandaoni. Number One inatajwa kuwa ndiyo kolabo hatari ya kufunga mwaka. Mpaka sasa ngoma hiyo ya audio ina kama wiki moja tangu itoke na ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2 pale YouTube huku ikishika namba tatu.

 

Pia imefanikiwa kushika namba tatu kwenye trending ya ngoma zote za Bongo Fleva. Kwa jinsi inavyokuja juu kwa kasi, inaweza kupindua Ushamba ya Harmonize ambayo inashikilia namba moja ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 3.

KIBA NA NANDY (NIBAKISHIE)

Nibakishie ni bonge moja la ngoma kutoka kwa King Kiba na Nandy. Kwa sasa Nibakishie inaendelea kupanda viwango kadiri muda unavyosonga.

Walianza kwa kuachia audio kwanza ambayo ndani ya siku 5 za kwanza imesikilizwa zaidi ya mara laki tano kisha wakaachia video yake ambayo ilikuwa inakimbilia watazamaji milioni 1 ndani ya siku moja. Ngoma hii inavyokuja kwa kasi, inabidi Number One ya Rayvanny na Zuchu ­ ipange la sivyo itapinduliwa.

 

MONDI, ROMMY JONES NA CEEZA MILL (ROTATE)

Rotate ni ngoma kutoka kwa Rais na Makamu wa Rais wa WCB, Mondi na Rommy Jons wakishirikiana na msanii kutoka nchini Nigeria, Ceeza Mill. Ni ngoma ambayo ni audio tu, lakini inafanya poa mpaka. Ina wiki moja tu tangu itoke na inawasikilizaji zaidi ya laki tatu.

HARMONIZE NA NAIRA MARLEY (USHAMBA REMIX)

Ushamba Remix ni ngoma kutoka kwa Jeshi ambaye pia ni mmiliki wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide. Kwenye ngoma hii ambayo Harmonize anatarajia kukiwasha muda wowote, ameshiri kiana na msanii kutoka Nigeria, Naira Marley.

 

Harmo nize amedokeza ujio wa Ushamba Remix wakati akielekea kwenye Tamasha la Harmonize Carnival ambalo litaanza tarehe 28, mwezi huu ndani ya Uwanja wa Uhuru j­ ini Dar. Ukiachilia mbali Ushamba Remix, jamaa huyo pia kwa sasa anatamba na Ngoma ya Ushamba inayofanya poa huko mjini YouTube ambayo mpaka sasa ina jumla ya watazamaji zaidi milioni 3 ndani ya wiki mbili.

 

MEJA KUNTA NA MALKIA KAREN

(SINA) Ngoma ya Sina inatoka kwa mkali wa Singeli, Khalid Sadick ‘Meja Kunta’ akiwa na sexy lady kunako Bongo Fleva, Karen Habash ‘Malkia Karen’. Ngoma hii ina siku chache tangu itoke, lakini inakimbiza na ipo kwenye ngoma zinazotrendi na jumla ya watazamaji zaidi ya laki tatu huku ikishika namba 10 pale mjini YouTube.

 

JUX NA OTILE BROWN (REGINA)

Hii ni o cial video kutoka kwa Jux akiwa na msanii kutoka nchini Kenya, Otile Brown. Ngoma hii kwa sasa ipo kwenye trending huko mjini YouTube ikiwa na jumla ya watazamaji zaidi ya milioni moja ndani ya wiki moja huku ikishika nafasi ya 20.

MONDI NA MBOSSO

Mondi na Mbosso nao wana jambo lao kwenye kufunga mwaka huu. Mbosso aliandika waraka kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba anatamani siku ziende waachie dude lao la pamoja.

Hii ina maana kwamba wawili hawa wana jambo lao siku siyo nyingi ambapo wanawaacha kwanza Rayvanny na Zuchu wasogee kidogo ndiyo wakiwashe. Mondi na Mbosso hawajawahi kufanya kolabo hata moja ndiyo maana kolabo yao inatajwa kwamba itafunga mwaka kwa kishindo.

 

Makala: Khadja Bakari, Bongo

 

 

Leave A Reply