OFM yanasa wagonjwa wakiosha vyombo kwenye masinki ya vyoo

Mayasa Mariwata na Haruni Sanchawa

HII kali! Hili ndilo neno linaloweza kusemwa baada ya wagonjwa wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kukutwa wakiosha vyombo katika sinki la vyoo, Risasi Mchanganyiko linathibitisha.

Kitengo cha Oparasheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kilifika katika jengo hilo na kufanikiwa kuingia wodi hiyo ya wazazi namba 33 ambako liliwakuta wagonjwa hao wakitumia sinki hilo linalotakiwa kutumiwa na watu watokao chooni, wakiosha vyombo vinavyotumika kwa chakula na matumizi mengine.

Inadaiwa kuwa sinki hilo ndilo ambalo pia wagonjwa hao hulitumia kwa kunawia mikono na kupigia mswaki, kitu kinachoweza kusababisha hatari ya kupatwa na magonjwa mengine nje ya waliyokwenda nayo.

Muuguzi mmoja wa wodi hiyo, aliyezungumza na OFM kwa sharti la kutotajwa jina, alisema hali hiyo imetokana na makosa ya wajenzi wakati wakifanya ukarabati wa jengo hilo miaka saba iliyopita, ambao walisahau kuweka sinki maalum kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa.

“Miaka kama saba iliyopita ulifanyika ukarabati sasa mafundi wakakosea hawakuweka sehemu ya kuoshea vyombo jambo ambalo ni tatizo na kero kwa wagonjwa,” alisema muuguzi huyo.

Gazeti hili lilimtafuta Emeniel Eligalesha, ambaye ni Afisa Habari Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili lakini simu yake haikupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakuweza


Loading...

Toa comment