The House of Favourite Newspapers

OPERESHENI YA KUKAMATA WEZI KAZI ZA WASANII YAENDELEA DAR

0

Askari wakikamata CD feki, eneo la Buguruni Sokoni, Dar.

Operesheni hiyo ikiendelea.

Kompyuta zilizokamatwa zikipelekwa kwenye gari la polisi.

 

OPERESHENI ya kuwakamata watu wanaodurufu CD feki za wasanii, leo imeendelea katika maeneo ya Kariakoo, Buguruni, Vingunguti na maeneo ya Tandika Sokoni ambapo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Kampuni ya Msama Promotions ambao ni wasimamizi na wasambazaji wa kazi za muziki wa Injili, chini ya mkurugenzi wake, Alex Mwita Msama walikuwepo katika operesheni hiyo.

Akizungumza katika  operesheni hiyo, Msama alisema kuwa, amekuwa akiwatahadharisha watu kuachana na kazi hiyo ya kudurufu CD feki, kuuza CD zisizokuwa na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivyo amesisitiza wanaodurufu CD hizo kuacha kazi hiyo au kufanya kazi iliyo rasmi ili serikali iweze kujipatia mapato na wasanii wanufaike na jasho la kazi zao.

Alisema serikali inatengeneza mazingira safi na wafanyabiashara waaminifu wanaofuata utaratibu sahihi, ukiwemo ulipaji wa kodi kwa wakati na hivyo kampuni yake itaendelea kuhakikisha kazi za wasanii zinalindwa na kuheshimika ipasavyo.

Pia, katika kuonesha msisitizo, Msama alisema; “Serikali ya awamu ya tano ni serikali ya kazi, hivyo haina chuki na mfanyabiashara yeyote anayefuata utaratibu wa kawaida ikiwemo kulipa kodi na mambo mengine ya kufanana na hayo.

“Nirudie tena wito wangu kwamba sasa biashara haramu ya kazi za wasanii basi na hii yote ni kutokana na kampeni yetu ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii na tutahakikisha tunawakamata wote watakaondelea na tabia hiyo nchi nzima tutawafikia,” alisema.

“Tukiwaondoa wezi wa kazi za wasanii serikali itakusanya kodi halali. Kwa kufanya hivyo wananyonya jasho la wasanii na kuiingizia hasara serikali kwa kutolipa kodi halali, naomba wadau wapenda maendeleo mnielewe,” alisema Msama.

Leave A Reply