The House of Favourite Newspapers

Paula Hajavunja Penzi la Rayvanny na Fahyma

0

KAPO inayozungumzwa zaidi ya staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny na Paula Kajala; imekuwa na mambo mengi.

 

Miongoni mwake ni Paula kuandamwa kwamba ndiye aliyevunja penzi la Rayvanny na baby mama wake, Faima Msengi au Fahyma.

 

Paula amekuwa akishambuliwa mno akitajwa kuwa chanzo cha wawili hao kutengana lakini, mtandao wa Global Pubishers umezama chimbo na kuibuka na ujumbe wa mwaka jana; miezi kadhaa kabla ya Rayvanny kutua kwa Paula.

 

Ujumbe huo unaonesha kuwa, Rayvanny na Fahyma walishatengana kabla ya jamaa huyo kutuliza mtima wake kwa Paula ambaye ni mtoto wa mastaa, mwigizaji Kajala Masanja na prodyuza P Funk Majani.

 

Ujumbe huo ambao nakala yake uliandikwa na Rayvanny kwenye ukurasa wake wa Instagram ukionesha kabisa mambo yalishaharibika siku nyingi kati yake na Fahyma.

 

“Nimekuwa ninakuheshimu miaka yote tuliyokuwa pamoja, kuna mengi tulikosena na tumesameheana na most of the time (wakati mwingi) umekuwa ukitamani maisha ambayo kila siku nakwambia hayatakusaidia… nakuheshimu na ninaheshimu sana familia yangu…ikiwa umeamua mwenyewe kuondoka I won’t blame you (sitakulaumu)…I still love my family (bado ninaipenda familia yangu…nakutakia maisha mema…” Aliandika Rayvanny na kumalizia na ishara ya shukrani.

 

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyouleta ujumbe huo wa Rayvanny, Fahyma ndiye aliyeamua kuondoka nyumbani kwa Rayvanny na kwenda kuishi kivyake.

 

Habari za ndani zinasema kuwa, baada ya Rayvanny kujiridhisha kwamba, Fahyma hawezi kurejea kwake ndipo akaanza kumpigia misele Paula ambaye miezi kadhaa baadaye; yaani mwanzoni mwa mwaka huu alifanikiwa kumuweka kwenye himaya yake.

 

Kwa sasa, Paula yupo masomoni nchini Uturuki wakati Rayvanny akiwa Bongo, jambo ambalo linatia shaka kwamba huwenda umbali huo unaweza kusababisha kusambaratika kwa penzi lao.

STORI; MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply