The House of Favourite Newspapers

Paula: Umefika Muda Sasa Niitwe Mama

0

RAYVANNY staa mwingine wa Bongo Fleva ambaye alianza ‘kudeti’ na mrembo Paula Kajala mwaka jana baada ya kuachana na baby mama wake, Fahyma.

Tangu hapo, Rayvann au Chui wamekuwa na vipindi tofauti ikiwemo kupostiana picha zao za kimahahaba na kupeana maneno matamumatu ya mapenzi ikiwemo kuitana ‘moyo wangu’.

Ukiachana na kapo ya Nandy na Nenga, basi Rayvanny na Paula nayo ni kapo inayofuatiliwa zaidi ndani na nje ya Bongo.

Mapenzi ulipoingia mwaka 2022, Paula aliyeko masomoni nchini Uturuki aliposti picha yake na kuandika; “Bonnie is ready…”

Bonnie ni jina la kimahaba ambalo Paula alipewa na Rayvanny akimaanisha yupo tayari hivyo baadhi ya mashosti zake wakasema alikuwa akimuambia jamaa huyo yupo tayari kupata mtoto.

Hata hivyo, baada ya kuona kama Rayvanny hakumuelewa, juzikati aliposti picha ya mwanamke mjamzito na kuandika; “Umewadia muda sasa niitwe mama…”

Baadhi ya watu wanadai huwenda tayari ni mjamzito au anategemea kubeba mimba hivi karibuni hivyo baadhi ya wafuasi wake kumpongeza kwa hilo na kumkaribisha kwenye ulimwengu wa akina mama.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply