The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli ‘Agomea’ Jukumu la Kunyonga Wafungwa

0
Rais Magufuli (katikati) akiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) na Prof. Ibrahim Juma mara baada ya kuapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma kutompelekea orodha ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ili aidhinishe kunyongwa kwao kwani anafahamu ugumu ulivyo wa kufanya hivyo.

Rais Magufuli ameyasema hayo katika halfa ya kumuapisha aliyekuwa Kaimu Jaji Mkuu kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania baada ya jana kuteuliwa rasmi kushika wadhifa huo.

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na Jaji Mkuu Mpya, Prof. Ibrahim Juma, Ikulu, Dar.

“Ninafahamu baadhi ya wafungwa hawa wapo wengi wanaosubiri kunyongwa hadi kufa, na marais waliopita walikwepa jukumu la kusaini sheria hii, na mimi nakuomba Jaji Mkuu usiniletee kwa sababu nafahamu ugumu wake,” alisema Rais Magufuli.

Tamko hilo la Rais Magufuli limeungwa mkono na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambapo wamesema kwamba sheria ya kifo inakiuka haki ya kuishi na inatweza utu wa binadamu.

 

Rais Magufuli (katikati) akiwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) na Prof. Ibrahim Juma mara baada ya kuapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewapongeza majaji wote waliopo kazini na wastaafu na kusema kwamba wanafanya/walifanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi.

Kwa upande wake Jaji Mkuu, miongoni mwa mambo mengi aliyoyazungumza ni pamoja na kutolea ufafanuzi taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa na watu kuwa kuna muingiliano katika mihimili ya serikali.

Akitolea ufafanuzi hilo alisema si kweli kwamba kuna muingiliano unaodaiwa, bali kuna wakati muhimili hiyo lazima ikae pamoja kuwatumikia wananchi lakini kila mmoja una majukumu yake ya kutekeleza.

 

Leave A Reply