The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aagiza Tozo za Mafuta Kupunguzwa

0

Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kupunguzwa kwa tozo zinazotozwa na taasisi mbalimbali katika bidhaa za mafuta nchini zenye thamani ya shilingi bilioni 102 kwa mwaka, kwa lengo la kupunguza bei za mafuta ili kuwapa unafuu wananchi.

 

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo, Iktoba 5, 2021 wakati akipokea taarifa kutoka kwa waziri wa nishati, January Makamba kuhusu utekelezahi wa maagizo aliyoyatoa kwa wizara hiyo kupitiamwenendo wa biashara yamafuta na bei zake nchini.

 

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, inaeleza kuwa utekelezaji wa maagizo hayo unaenda sambamba na marekebisho ya kanuni mbalimbali zinazohusiana na tozo na yatachapishwa katika Gazeti la Serikali.

Leave A Reply