The House of Favourite Newspapers

Paula Alia… Nitakonda Sana Huku

0

PAULA Kajala ambaye mpenzi wa msanii Rayvanny ametoa kauli ya kushtua akisema; “Nitakonda sana huku niliko!”

 

Inafahamikwa kwamba, Paula amekwenda kusoma nchini Ukraine na kumuacha mpenzi wake huyo Bongo katika kipindi ambacho gari la penzi lao limewaka.

 

Kilio hicho cha Paula kimeibua mambo mazito kwani kimekuja mara tu baada ya kuenea kwa madai kwamba huwenda Rayvanny akarudisha majeshi kwa baby mama wake, Fahyma.

 

Madai ya Rayvanny kurejea kwa Fahyma yamekuja kufuatia mwanamama huyo kuonekana akisafiri kuelekea jijini Arusha akiwa amevaa koti linalosemekana ni la jamaa huyo.

 

Kupitia kipande cha video, Paula amesema; “Lazima nitakonda sana huku, kisa maisha magumu.”

Kauli hiyo ya Paula inaelezwa kuwa, kitakachomkondesha ni drama zinazoendelea zikimhusisha Rayvanny na Fahyma.

 

Hata hivyo, Paula ameendelea kuposti video za siku za nyuma zikimuonesha akiwa na Rayvanny na kurusha vijembe.

Baadhi ya watu wamedai kwamba, drama hizo zitamsababishia Paula ashindwe kusoma kwa sababu mtu akishajihusisha na mapenzi ni ngumu kusoma na mbaya zaidi ni kwamba mapenzi ya mbali hawatayaweza.

 

Watu wengine wanasema kuwa, kusudi la Fahyma ni kumvuruga kabisa Paula ili ashindwe kusoma na ndiyo maana kwa sasa anafanya mahojiano mbalimbali akimsifia Rayvanny.

 

Katika moja ya intavyu hizo ambazo zinadaiwa kumrusha roho Paula ni pamoja na ile ambayo anasema kuwa, licha ya kuachana na Rayvanny, bado anaendelea kumsifia baba mtoto wake huyo kwa sababu ni mtu aliyekamilika na muhimu sana kwa upande wake.

 

Fahyma anasema; “Bado naendelea kumsifia, ni mtu aliyekamilika sana kwangu mimi sijui kwa wengine ila kwangu bado ni mtu muhimu sana kwa sababu roho ya mtoto wangu ni yangu pia.”

Fahyma anamtaja Rayvanny kuwa ni baba bora kwa mtoto wao wa kiume aitwaye Jaydan.

 

Anafafanua kuwa, Rayvanny anamjali mtoto wake sana na wana muunganiko ulio bora.

Fahyma na Rayvanny waliachana mwaka jana baada ya kuwepo kwa madai ya kusalitiana, jambo ambalo mwanamama huyo amelikanusha akisema hajawahi kumsaliti jamaa huyo.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

 

Global App

Android Google Play: Bofya Hapa

iOS App Store: Bofya Hapa

Leave A Reply