The House of Favourite Newspapers

Shazam Yazindua Playlist ya Mastaa Afrika Mashariki Ndani ya Apple Music

0

SHAZAM imezindua playlist yake mpya ya wasanii wanaofanya vizuri Afrika Mashariki katika Mtandao wa Apple Music, ijulikanayo kama East Africa Risers ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zinazotamba Kenya, Tanzania na Uganda.

 

 

 

Jukwaa hilo halitakuwa na nyimbo za wasanii pekee, bali pia litajumuisha nyimbo zinazotumika kwenye filamu kama sound tracks, kwenye runinga na nyimbo zinazotrend kwenye mitandao ya kijamii.

 

 

Playlist ya East Africa Risers ni mjumuisho wa nyimbo zinazotamba katika jukwaa la Shazam katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

 

Itakuwa inatoa mchanganyiko wa nyimbo zinazoonesha jinsi nguvu ya muziki inavyovuka mipaka ya Afrika Mashariki, kuanzia Afrobeats na Bongo Flava mpaka Afro-Pop na Hip-Hop.

 

 

Playlist hiyo itajumuisha nyimbo za wasanii wanaokuja kwa kasi, Zuchu na Nandy na mastaa wa Afrika Mashariki, Rayvanny na Harmonize.

 

 

“Nina furaha kubwa kuwa miongoni mwa wasanii wa mwanzo watakaojumuishwa kwenye playlist ya Shazam East Africa Risers. Ni baraka kubwa kwangu na nataka kuwashukuru timu yangu na mashabiki kwa kuendelea kuunga mkono juhudi zangu pamoja na Shazam ambao wamekuwa mstari wa mbele kuwasaidia mashabiki kuujua muziki wangu kwa urahisi,” anasema Nandy.

 

 

Playlist ya Shazam East Africa Risers itakuwa inawekwa nyimbo mpya kila wiki na itakuwa inapatikana kwenye jukwaa la Apple Music pekee. http://apple.co/EastAfricaRisers

 

 

Shazam ni moja ya programu maarufu za muziki na zinazopewa hadhi ya juu duniani na inawaruhusu watumiaji kutambua nyimbo kwa kusikiliza muziki unaochezwa karibu nao au kwenye kifaa chochote. Pamoja na uvumbuzi, Shazam husaidia watu kugundua, kuingiliana na kushiriki video au sauti kwenye vifaa mbalimbali.

Leave A Reply