The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Si Kila Aliyeacha Shule Alikwenda Kuwa Bilionea – Video

0

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo.  amewasihi wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini College (TUDARCo) kujituma katika masomo yao kwani elimu ni kitu muhimu sana katika maisha yao ya sasa na ya baadaye.

 

Shigongo ameyasema hayo jana, Desemba 20, 2019, usiku wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza iliyofanyika chuoni hapo ikiambatana na tukio la kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri kwenye shindano la Public Speaking.

 

“Kama ulikuwa na mashaka kuhusu Chuo Kikuu cha Tumaini basi ondoa mashaka hayo, kama mimi umenikuta nasoma hapa, basi elewa kwamba chuo hiki ni moja ya vyuo bora sana hapa nchini. Wengi huniuliza kwa nini nimeamua kuacha vitu vyangu vyote nikarudi darasani na kukaa kwenye dawati nikafundishwa na mwalimu, nikafanya assignments na kusoma kwa bidii, jibu langu ni kwamba elimu ni muhimu sana kwangu.

 

“Huwa tunasikia huko kwamba matajiri wengi wakubwa wa dunia waliacha shule wakawa mabilionea, si kila aliyeacha shule akaenda kufanya biashara alikwenda kuwa bilionea, ni wachache sana waliofanikiwa kwa njia hiyo. Niwaambie tu ukweli ni kwamba, elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu.

 

“Tumekuja hapa chuoni ili kujifunza na tukirudi huko tuwe na uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali za maisha yetu, iwe kwenye ajira, ndoa, biashara ama matatizo ya nchi yetu,” amesema  Shigongo.

 

MANENO YA ERIC SHIGONGO KWA WANACHUO WA TUDARCO

Leave A Reply