The House of Favourite Newspapers

Shilole Afunguka Sababu ya Kuzirai Akivalishwa Pete

0

MSANII wa Bongo Fleva na mjasiriamali maarufu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’,  amenyoosha maelezo kufuatia ‘surprise‘ aliyofanyiwa kwa kuvalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake #Rommy, hali iliyopelekea kuzimia wakati linafanyika tukio hilo kwenye ‘birthday party’ yake.

 

#Shilole amesema hakutegemea na hakuamini kama atavalishwa pete hiyo ya almasi na mwanaume ambaye amempambania kwa nguvu zote.

 

“Sikutegemea na sikuamini kabisa, nilikuwa na taharuki na nilishtuka kwa kweli kwa sababu haikuwa tegemeo maana mimi nilikuwa na jambo langu mwenyewe la kujizawadia gari hata mwanamme mwenyewe hakuwa na dalili ya kunivalisha pete, pia sikuwa nimefikiria hivyo vitu, ila sasa hivi hapa nina pete yangu ya almasi kwenye kidole changu,” amesema.

 

Aidha,  amesema yupo tayari kwa ndoa ya pili na ikimpendeza Mungu basi wataoana kwa sababu kuolewa kwa mwanamke ni sunnah.

Leave A Reply