The House of Favourite Newspapers

TCRA: Mafundi Simu, Nendeni Mkasome

0

SERIKALI imesema ipo katika mchakato wa kutunga sheria itakayoweka utaratibu wa mafundi simu kusoma taaluma hiyo vyuoni na kupata cheti ili waweze kupata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

 

Mafundi hao watatakiwa kusoma katika vyuo vinavyotambulika kikiwemo cha ufundi (Veta) na DIT ili kupata leseni kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo.

 

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa leseni na ufuatiliaji wa TCRA, John Daffa katika mahafali ya tisa ya chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-Veta Kipawa.

 

Daffa amesema Serikali ilitoa udhamini wa masomo kwa baadhi ya mafundi simu Tanzania bara na Zanzibar ili iwaamshe wengine kwenda kusoma.

 

Amesema siku zijazo kutakuwa na sheria itakayowabana mafundi hao ambao watatakiwa kuwa na vyeti vya mafunzo ya ufundi simu ili waweze kupata leseni.

 

“Katika uanzishwaji wa sheria yoyote lazima utoe muda wa wahusika kupata elimu na ndio maana Serikali iliamua kudhamini baadhi ya mafundi kwenda kusoma kozi hiyo lakini ukweli ni kwamba haiwezi kudhamini mafundi wote waliopo nchini ila tumefanya mfano kwa hao wachache ili iwahamasishe wengine kufanya hivyo.”

 

“Hivyo mafundi changamkeni katika hili kwani itafika mahali hamtaweza kufanya kazi hiyo bila cheti kitakachokuwezesha kupata leseni kutoka TCRA,” amesema.

 

Leave A Reply