The House of Favourite Newspapers

Tambwe Alilia Kusajiliwa Yanga SC

0

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amefunguka kuwa bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hivyo uongozi wa Yanga uende ukamsajili.

 

Tambwe ambaye aliwahi kutamba na klabu za Simba na Yanga, amesema anatamani kurudi Yanga kwa sababu ni timu ambayo anaipenda, lakini mbali na hivyo anataka kutatua ukame wa mabao kwenye klabu hiyo kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo bado anao.

 

Tambwe ambaye kwa sasa hana timu, yupo nchini tangu wiki iliyopita, ambapo ameshapata nafasi ya kuishuhudia Yanga ikicheza michezo miwili, dhidi ya Simba na pia dhidi ya KMC.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe alisema, bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hivyo uongozi wa Yanga usisite kumrejesha kundini kwa kuhofia kiwango chake, huku akienda mbali zaidi kwa kusema yeye ni mmoja wa watu ambao wanaipenda sana klabu hiyo.

 

“Bado nipo vizuri, sina mzaha nikiwa kwenye lango, Yanga wakinisajili nitawafanyia kazi kweli, unajua mimi nina mapenzi na Klabu ya Yanga, kwa hiyo nikirejea hapo nitaipambania kwa moyo wote,” alisema Tambwe.

IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply