The House of Favourite Newspapers

TAMWA Wakemea Rushwa ya Ngono Na Unyanyasaji Katika Vyombo vya Habari

0

Kuelekea safari ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kijinsia, Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Dkt. Rose Reuben amezungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Leo Novemba 22, 2023 na kueleza dhamira ya mkutano huo ni kukemea suala zima ukatili wa Rushwa ya Ngono na unyanyasaji wa kingono ndani ya vyombo vya habari.

TAMWA kwa kuonesha msisitizo katika hilo wamekuja na kauli mbiu inayosema ‘wekeza kuzuia Ukatili wa Kijinsia’ kauli mbiu hii imeambatana na kutoa elimu kwa watu mbali mbali ili wavunje ukimya pindi wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia.

Aidha TAMWA kuelekea maadhimisho haya iliweza kufanya mambo kadhaa kama ifuatavyo:


Mosi, Kuvunja ukimya uliotawala miongoni mwa wanahabari katika kusema kinagaubaga au kuandika kuhusu madhala wanayopia wanapodhalilishwa kingono.

Pili, TAMWA imebaini asimia 48 waliohojiwa tu ya wanahabari ndio wanaweza kusema wazi kuhusu madhala ya Rushwa ya ngono. Tatu, TAMWA imebaini kuwa wanahabari wengi wanawake wameacha kazi kwa kuhofia udhalilishaji wa kijinsia katika tansia hiyo.

Nne, wapo viongozi katika maeneo ya kazi, wanatoa kazi kwa upendeleo kwa kuomba rushwa ya ngonobadala ya kuangalia uweezo na vipaji na kwa nguvu kubwa wanajitahidi kuficha ukweli wa uvunjifu wa maadili wanaoufanya.

Akihitimisha katika mkutano huo Mkurugenzi wa TAMWA Dkt. Rose Reuben ameitaka jamii kufunguka na kutofubia macho jambo hili kwani liaathiri kizazi na kizazi na wakati mwingine kupelekea kifo kwani baadhi yao wanaofanyiwa ukatili huu huchukua jukumu la kujinyonga na hatimaye kupoteza maisha.

Leave A Reply