The House of Favourite Newspapers

Tume ya Haki za Binadamu: Waliobomolewa Buguruni Wameonewa, Lazima Walipwe

0
Bahame Nyanduga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari.

 

Nyanduga akifafanua jambo

 

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, imesema kwamba ubomoaji wa nyumba katika eneo la mita 30 kutoka kwenye reli, haukuwa wa halali na kwamba, wote waliobomolewa, wanatakiwa kulipwa fidia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao, Magogoni jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga alisema tume yake ilipokea malalamiko Februari 23, 2017 kutoka kwa kamati ya waathirika wa Kata ya Mnyamani ambapo baada ya kufuatilia malalamiko hayo, wamebaini kwamba kulikuwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.

Nyanduga aliongeza kwamba, nyumba zilizopo umbali wa mita 30 kutoka kwenye reli, zilibomolewa kimakosa na kwamba serikali kupitia Shirika Hodhi la Reli (Rahco), inatakiwa kuwalipa fidia wote waliobomolewa nyumba zao na kwamba itahakikisha inachukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika na zoezi hilo la ubomoaji.

Leave A Reply