The House of Favourite Newspapers

Tuwatimue Wamachinga?

0

TANZANIA bado ina uchumi legelege, asilimia kubwa ya wananchi wake ni masikini.
Ajira limekuwa jambo la bahati; kwa mwaka vijana wanaopata ajira ni 40,000 kati ya Milioni Moja wanaohitimu masomo kutosha shule na vyuo mbalimbali.

 

Hii ina maana kwamba, vijana 960,000 wanaishi kwa kujiajiri kwa kilimo na biashara ndogondogo; si aibu kuliita taifa hili kuwa ni taifa la “Wamachinga” ambao kwa sasa hawatakiwi kuishi mijini.

 

Baadhi ya watu wamekuwa watengeneza hisia hasi kuhusu Wamachinga kwamba maisha yao yapo kwa ajili ya kuchafua miji, kuhatarisha maisha ya watu wengine, kuzuia biashara za watu zisifanyike kwa uhuru na pengine kujihatarishia usalama wao wenyewe.

 

Kuna msemo wa Kingereza unasema “Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.”
Je, tunakusudia kuwaua ndugu zetu kwa kuwapa majina mabaya yakiwemo ya kuuza chakula kwenye transifoma za umeme kana kwamba miji yote imejaa transifoma?

 

Jibu ni hapana; kwani Wamachinga ni ndugu zetu watoto wa taifa hili wenye haki ya kuishi kwa uhuru katika nchi aliyowapatia mwenyezi Mungu.

Niko hapa kuitisha mjadala, nini kifanyike ili Wamachinga waweze kuishi na kufanya kazi zao kwa uhuru kwani hayo ndiyo maisha yao na familia zao.

 

Kumfukuza Mmachinga mjini wakati hajapewa ajira, hajawezeshwa kiuchumi ni kumkosea, ndiyo maana nataka maoni yao mdau wa Global uiambie serikali nini cha kufanya ili Wamachinga wapate uhuru wao wa kufanya shughuli ambazo zinawafanya wasomeshe watoto na kulea familia zao?

 

Weka maoni hayo hapa chini! Kesho tutaendelea kutoka tutakapoishia.
@manyota_rich

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply