The House of Favourite Newspapers

Uchebe Kortini kwa Kumpa Vipigo Shilole

0

ASHRAFU GEUZA  maarufu ‘Uchebe’,  amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na kosa la kumjeruhi mkewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu ‘Shilole’,  na kumsababishia maumivu.

 

Wakili wa Serikali, Chesensi Gavyole,  amedai kuwa Julai 6, 2020, maeneo ya Ada Estate Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  mshtakiwa alimpiga Shilole sehemu ya kichwa na shingoni na kumsababishia maumivu makali.

 

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka linalomkabili na yupo nje baada ya kukidhi masharti ya dhamana. Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23, 2020 kwa ajili ya usikilizwaji.

 

Leave A Reply