The House of Favourite Newspapers

UN: Israel Yataka Watu Milioni 1.1 Gaza Kuondoka Katika saa 24 Zijazo

0

Jeshi la Israel limeuambia Umoja wa Mataifa kwamba kila mtu anayeishi kaskazini mwa Wadi Gaza anapaswa kuhamia kusini mwa Gaza katika muda wa saa 24 zijazo, anasema msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa unasema kiasi hiki kinafikia takriban watu milioni 1.1 – karibu nusu ya wakazi wa Ukanda wote wa Gaza.Eneo lililoathiriwa ni pamoja na Mji wa Gaza wenye wakazi wengi.

Tahadhari hiyo ilitolewa kabla tu ya usiku wa manane, saa za Gaza na Jerusalemu (23:00 GMT).

“Umoja wa Mataifa unaona kuwa haiwezekani kwa harakati kama hiyo kufanyika bila matokeo mabaya ya kibinadamu,” Umoja wa Mataifa ulisema katika taarifa yake.

Israel imekuwa ikijiandaa kwa mashambulizi ya ardhini, kukusanya wanajeshi, mizinga mikubwa na vifaru kwenye mpaka wa Gaza.

Imekuwa ikiafanya mashambulizi ya anga mjini Gaza tangu Jumamosi baada ya wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel kwa kushtukiza.

MFANYABIASHARA MAARUFU ARUSHA AFIA NDANI ya GARI- AKUTWA na MABURUNGUTU ya PESA SIKU ya 5..

Leave A Reply