The House of Favourite Newspapers

Utoaji wa Tuzo za Grammy 2022 Zaahirishwa

0

Tuzo za 64 za Grammy zilizokuwa zikitarajiwa kufanyika januari 31 mwaka 2022, zimeahirishwa kutokana na kuongezeka kwa kesi za Covid-19 huko nchini Marekani.


Kwa mujibu wa waandaji wa tuzo hizo zenye heshima kubwa Duniani, Siku ya jumatano waliweka wazi kuwa tukio hilo litapangwa upya na tarehe yake itatangazwa rasmi mapema baada ya kujiridhisha na kupungua kwa kesi za kuenea kwa Covid-19.


Tuzo hizo zilipangwa kufanyika huko Los Angeles nchini Marekani. M
chakato wa uteuzi wa washiriki wa tuzo hizo ulitangazwa mnamo Novemba 23 2021. Ambapo wasanii kadhaa walitajwa kuwania kwenye vinyang’anyiro mbalimbali.


Wasanii kama Justine bieber na H.E.R ni miongoni mwa wasanii wa waliotajwa zaidi kwenye vipengele takribani nane, huku rapa Jay z akiingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuwa msanii aliyeteuliwa zaidi katika historia ya onesho hilo.

Leave A Reply