The House of Favourite Newspapers

Mbowe, Lema na Mbatia Wakicheza Blues (Pichaz + Video)

0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe akicheza na bi. harusi.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia nae akicheza muziki.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akifanya yake.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akicheza muziki na mwenzake.
Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema akicheza na mke wake.
Mbowe akicheza muziki

Joseph Haule ‘Profesa Jay’ amefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Grace Mgonjo. Ndoa ya Prof Jay ambaye ni Mbunge Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ilifungwa mchana wa Jumamosi, JULAI 08, 2017, katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar na usiku mpango mzima ulihamia kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo mastaa wa muziki na filamu sambamba na wanasiasa, wengi wakiwa ni wabunge na viongozi wa Chadema walifurika.

Ulipofika muda wa kufungua muziki, Profesa Jay na mkewe walitia fora kwa kucheza ‘blues’ taratibu na kuwa kivutio kikubwa ukumbini hapo. Yote tisa, kumi ni pale waheshimiwa wabunge walipoanza kuyarudi, kila mtu na wake. Ilikuwa hapatoshi.

Profesa Jay, kabla ya ndoa hiyo, yeye na Grace wamejaliwa mtoto mmoja wa kike.
Shoo ya Diamond kwenye harusi hiyo ilibamba mno na kuwafanya wanakamati wawe na kazi ya ziada ya kutuliza watu watulie kwenye siti zao.

(PICHA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS)

Leave A Reply