The House of Favourite Newspapers

Wanaodaiwa Kumuua Mama Yao Mzazi Wanaswa

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia watu watatu wa familia moja kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya mama yao mzazi, Frazia Rukera mwenye umri wa miaka 99, mkazi wa Kijiji cha Mkombozi kata ya Rukuraijo wilayani Kyerwa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Tuntufye Mwakagamba amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Laurent Frances mwenye umri wa miaka 60, Alexander Francis mwenye umri wa miaka 55 pamoja na Agness Gidioni mwenye umri wa miaka 70, wote wakazi wa Kijiji cha Nyabirungu wilayani Kyerwa.

 

Kamanda Mwakagamba amesema watuhumiwa hao, wanashikiliwa kwa sababu walikuwa na ugomvi wa muda mrefu uliotokana na kumtuhumu mama yao kuwa mchawi na kuongeza kuwa marehemu aliuawa kwa kukatwakatwa kwa kitu chenye ncha kali kisha kukatwa kichwa, mikono na miguu, usiku akiwa amelala ndani ya nyumba yake.

 

Leave A Reply