The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Anusurika Kuuawa

0

WAZIRI Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok, amenusurika kuuawa baada ya msafara wake kushambuliwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

 

Kupitia televisheni ya taifa ya Sudan vyombo vya usalama vimetangaza  kuwa Hamdok yupo salama na amepelekwa katika eneo lenye  usalama mkubwa.

Had sasa hakuna mtu au kundi lolote ambalo limedai kuhusika na jaribio hilo la mauaji ya kiongozi huyo.

 

Hamdok aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Sudan mwezi Agosti mwaka 2019, baada ya maandamano ya kudai demokrasia kulilazimisha jeshi kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Omar al-Bashir na kukabidhi uongozi wa serikali kwa raia.

Karibu mwaka mmoja baada ya Bashir kuondolewa madarakani, Sudan inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi.

 

Leave A Reply