The House of Favourite Newspapers

Yanga na Simba Kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru

0

Nina rafiki yangu anaitwa Kazua leo asubuhi kanipa kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru. Wakati wa ujana wake Kazua alikuwa mkoba, yaani “centre half,” wa Dundee United.

 

Leo mimi na sahib yangu Kazua akitutokea simba ghafla tumeliwa. Miguu hainyanyuki ardhini haitaki inatukatalia sharti tuibembeleze.

 

Mzee Mangara Tabu alikuwa President wa Yanga na Ayubu Kiguru alikuwa shabiki mkubwa sana wa Sunderland na unaweza kusema ndiyo Haji Manara wa enzi hizo.

 

Haji mwanafunzi kwa Ayubu.
Ayubu alikuwa na kipaji cha ajabu.

Mtu wa vibweka lukuki.

 

Sunderland ikichukua kikombe asubuhi anakujanacho sokoni anakiweka mbele ya ubao wake washabiki wa Sunderland wakija sokoni wanatunza.

Hapo chini soko la Kariakoo kama lilivyokuwa enzi hizo.

Hapo Ayubu kavaa jezi no. 6 ya Hamisi Kilomoni. Jioni soko likifungwa anahesabu fedha zilizotunzwa anapeleka club Congo na Mchikichi.

 

Soko zima lile limejaa wanazi wa Yanga basi Ayubu peke yake anapambananao na mwisho wa siku wanasalimu amri wanafunga virago hao wanaondoka.

 

Ayubu alikuwa ana ubao wa biashara Kariakoo Market. Siku hiyo Mzee Mangara kenda sokoni kununua mahitaji yake.

 

Ayubu kumuona Mzee Mangara akamuamkia kisha akamwambia, “Mzee Mangara kanunue hiliki tu basi. Vingine vyote vilivyobakia njoo uchukue kwangu bure.”

 

Yanga ilikuwa imefungwa na Sunderland. Mzee Mangara akamshukuru Ayubu kisha akamwambi, “Tutakutana Ilala Stadium.”

 

Ayubu akamjazia vitu Mzee Mangara kwenye jumu lake, Mzee Mangara akimshukuru Ayubu akashika njia kwenda nyumbani kwake ambako hapakuwa mbali na sokoni.

 

Leave A Reply