The House of Favourite Newspapers

Zuchu Amfunika Kiba

0

Msanii anayekuja kwa kasi kunako gemu la Bongo Fleva, Zuhura Othman Kopa ‘Zuchu’, amewafunika wasanii wengine wengi akiwemo Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’.

 

Kwa mujibu wa mtandao wa kupima kazi za wasanii (social blade), mrembo huyo amemfunika Kiba kwa nyimbo zake kutazamwa na watu wengi zaidi katika mwezi Julai. Takwimu hizo zinaonesha, Zuchu ametazamwa na watu 7, 260, 888 huku Kiba akiwa ametazamwa na watu 1,375,378.

 

KWA NINI AMFUNIKE KIBA?

Miongoni mwa maswali ambayo watu wengi watakuwa wanajiuliza kuwa kwa nini mrembo huyo amfunike Kiba ikiwa ana muda mchache tu kwenye gemu, Risasi lilizungumza na mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano, Edwin Lindege ambaye alitegua kitendawili hicho.

 

Lindege alisema, Zuchu amemfunika Kiba kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaotazama muziki wake.

“Unajua kinachosababisha mtu mmoja awe mkubwa zaidi ya mwingine, kwanza kabisa ni views (watazamaji) ambao wanakuwa wanatazama video zako, lakini jambo la pili ni ongezeko la subscribers (wafuasi) waliokufuata kwa mwezi husika.

 

“Tunaona watu waliom-subscribe Zuchu kwa mwezi mzima wa Julai, walikuwa ni 56,000 huku Alikiba akiwa na subscribers 13, 000,” alisema Lindege na kuongeza:

 

“Jambo la tatu ambalo ndilo muhimu kuliko yote, ni watch time (muda ambao video zako zimetazamwa) unajua kuna ile mtu anaweza akaingia tu kwenye video yako kisha akatoka halafu kuna wale ambao wanaingia kuangalia video yako mwanzo mpaka mwisho, hii ndio tunaita watch time yenye thamani ambayo inamfanya msanii video yake ionekane imetazamwa zaidi.”

 

Zuchu ana takriban miezi minne tangu aingie kwenye gemu la Bongo Fleva, huku Kiba akiwa mkongwe mwenye zaidi ya miaka kumi kwenye muziki huo.

Stori: Memorise Richard, Risasi Mchanganyiko

Leave A Reply