The House of Favourite Newspapers

Zuchu Awa Tishio Kwa Mastaa wa Kike Bongo

0

KAMA ameiona njia usiku, mchana ni ganda la ndizi, full kutereza; ndivyo itakavyokuwa kwa msanii Zuhura Kopa ‘Zuchu’.

Uchunguzi unaonesha kuwa msanii huyo ambaye ni memba wa mpya wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ambaye aliweza kuchomoka kimuziki na kuwa tishio kipindi ambacho kasi ya Corona ilikuwa kubwa, anaweza kuoga utajiri nyakati hizi ambapo shughuli zote za kijamii zimefunguliwa na Serikali.

 

Zuchu ambaye Aprili mwaka huu alisajiliwa WCB, aliweza kufyatua nyimbo kali na kujipatia fedha kwenye mitandao huwenda kasi ya kupiga ‘mpunga’ mrefu ikaongezeka mara dufu atakapoanza kufanya shoo na matamasha mengine.

“Kwenye mtandao wa YouTube ameweza kutikisa na kupata fedha, namuona akipaa kisanii wapinzani wake wajipange, vinginevyo watarajie kupewa lifti na Zuchu,” mmoja aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

Kwa kipindi hiki kifupi tena chenye giza la Virusi vya Corona, Zuchu alifanikiwa kuwa tishio kwa mastaa wengine wa kike Bongo kama Faustina Charles ‘Nandy’, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Vannesa Mdee ‘V Money’ na Mariane Mdee ‘Mimi Mars’ na wengine kibao.

 

Kuchomoka kwa staa huyo wa kike kumetabiriwa na wengi kuwa huenda anakwenda kuwa malkia wa Bongo Fleva kama alivyokuwa msanii Lady Jaydee miaka kadhaa iliyopita.

MAMBO ALIYOYAFANYA

Kipindi chote cha janga la Corona, Zuchu aliweza kuachia Extended Playlist (EP), yake ambayo ilikuwa imekusanya nyimbo sita na zote zilifanya vizuri katika mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watazamaji lukuki.Kishindo cha aina yake alikiweka YouTube ambapo kwa muda mfupi kazi zake zimetazamwa mara Milioni 12 ndani ya muda wa miezi mitatu tu na kumfanya Zuchu kama Zuchu kuwa juu.

Aidha, hivi karibuni aliweza kuishika Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuachia ngoma iitwayo Tanzania ya Sasa.Katika wimbo huo ambao uliwashika vilivyo viongozi wa serikali umejaa mashairi yenye kusifia mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya Magufuli.“Elimu ya msingi na sekondari bure Magufuli huyooReli yenye viwango bora standadi geji karibu inakamilika, Magufuli Hai“Baadhi ya viongozi walionesha kuvutiwa na ngoma hiyo, na kumsifia hadharani Zuchu, ni Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala.

 

SHOO MPYA

Kwa kipindi chote cha tishio la Corona na ujio wake msanii huyo hakuweza kufanya shoo yoyote, lakini baada ya Corona kufifia staa huyo chipukizi atafungua pazia lake la makamuzi jukwaani Juni 18 mwaka huu.Zuchu sambamba na menejimenti yake wameandaa shoo ya kufa mtu, siku hiyo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambapo anatarajia kuvuna fedha ambazo huenda hajawahi kuzipata tangu amezaliwa.Inaonekana kuwa baada ya Zuchu kuonja utamu wa shoo huenda ndiyo ikawa safari moja ambayo itaanzisha nyingine.

 

MENEJIMENTI ITAMBEBA

Zuchu ni msanii ambaye amefanikiwa kuwa na menejimenti makini inayomsimamia, ambayo imetajwa mara kadhaa kuwa ndiyo inayomvusha kwenye msitu wa sanaa.Menejimenti hiyo ambayo iko chini ya Hamisi Tale ‘Babu Tale’, Said Fella ‘Mkubwa Fella’, pia inasimamia kazi za msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye ni bosi wa Zuchu, kwa mkono mwingine imekuwa na mipango mathubuti pamoja na platifomu ya kutosha kwenye mitandao ya kijamii ambayo ikiamua kufanya jambo, halishindikani.Ingawa hali ya Corona haijatulia dunia nzima, lakini kipindi hali itakapokuwa nzuri upo uwezekano wa Zuchu kuvuka mipaka ya nchi na kuwa msanii wa kimataifa.Waandishi: Happyness Masunga na Khadija Bakari

Leave A Reply