The House of Favourite Newspapers

Bibi Miaka 68 Asimulia Alivyowashinda Majambazi 4 Mchana, Kuitwa Jeshini – Video

0


Rose Yoramu (68) ni mwanamke ambaye ni mlinzi wa ‘yard’ kubwa ya magari iliyopo Mikocheni kwa Warioba.

Akizungumza na Global TV, amesema kuwa anamshukuru Mungu tangu aanze kazi ya ulinzi mpaka sasa, ikiwa ni takribani miaka 30 ya kufanya kazi ya ulinzi hajawahi kuvamiwa zaidi ya yeye kukamata majambazi.

Bibi huyo ambaye si rahisi kugundua kuwa ni mlinzi unapomkuta kwenye lindo lake, amesema kuwa anajivunia na kazi hiyo imeweza kufanya akawa anaendelea kuishi japokuwa anapata kipato kidogo cha kumsaidia yeye na familia yake.

Leave A Reply