The House of Favourite Newspapers

Familia Yatupiwa Vyombo Nje na Kukosa Makazi – Video

0

TUKIO la kustaajabisha limetokea eneo la Mji Mpya Kipawa jijini Dar ambapo familia ya Bw. Abiud imekumbwa na kadhia ya kutolewa nje vyombo vyao na kukosa makazi kwa kile kilichoelezwa kuwa kutokana na mkopo wanaodaiwa na Benki.

 

Kwa mujibu wa Bw. Abiud amesema yeye alikopa kiasi cha Tsh milioni 10 na amesharejesha Tsh milioni 6 lakini benki hiyo imedai kuwa riba imepanda na kwa sasa inamdai Tsh milioni 14.

 

Abiud amesema thamani ya nyumba yake ni Tsh milioni 130 lakini anachoshangazwa nacho ni benki hiyo ni kutangaza kuipiga mnada nyumba yake kwa gharama ya shilingi milioni 20 kipindi yeye yupo safarini mkoani Morogoro.

Tazama tukio hili full kupitia Global TV Online ufahamu undani wake.

Leave A Reply