The House of Favourite Newspapers

FOA ya Mondi, Madee na Roma watia neno

0

Madee au Rais wa Manzese Music na Roma Mkatoliki, wamekuwa ni watu wa kutaniana mno kiasi kwamba kama hujui ni utani unaweza ukakurupuka na kudai wana ugomvi.

Sasa; Madee na Roma wameendelea utani wao, kila mmoja akijaribu kutoa kirefu cha EP (albam fupi) ya Diamond Platnumz ya FOA kwa kumtumia mwenzake ambapo utapenda majibizano yao.

Madee ndiye aliyeanza kuposti picha ya Roma kwa kuandika; Faster Ondoka America (ikumbukwe Roma kwa sasa anaishi Maremani).

Naye Roma akajibu hilo kwa kuandika; FATHER OA AISEE!! (Ikumbukwe Madee bado hajaoa).

Leave A Reply