The House of Favourite Newspapers

Harmo Kumburuza Wolper Kortini

0

TUSI la kishari la msanii Jacqueline Wolper Massawe alilomvurumisha mpenzi wake wa zamani Rajabu Abdul Kahali ‘Harmo’ huwenda likamtia matatani, Risasi limedokezwa.

Wolper kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni aliandika lugha ya matusi kwa Harmo ambayo gazeti hili haliwezi kuyanukuu.

 

Chanzo chetu kimesema kuwa Harmo amechukizwa na kitendo hicho na kwamba anafikiria namna ya kumburuza mahakamani mpenzi wake huyo wa zamani.

“Hata mimi siamini kama aliyeandika tusi hilo ni Wolper kwa sababu ni zito, kwa sasa Harmo yuko bize na kazi zake.

 

“Lakini amekasirika kwa vile hahusiki na chochote na hajui kwa nini Wolper aliandika tusi lile.

“Kuna baadhi ya rafiki zake nikiwemo mimi nimemshauri amshtaki ili kumtia adabu na yeye amesema anaangalia busara zake,” kilisema chanzo chetu ambacho kiko karibu na Harmo.

 

Harmo alipotafutwa na mwandishi wetu hakupatikana na meneja wake Beuty Mmari mara kadhaa amekuwa akisita kujibu masuala binafsi yanayomhusu msanii wake.

Hata hivyo, baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wameonesha kusikitishwa kwao na kitendo cha Wolper kumtusi mpenzi wake huyo wa zamani.

 

“Huyu amechoka kuishi uraiani anataka kwenda jela,” aliandika mtu mmoja kwenye mtandao wa kijamii huku mwingine akiweka ujumbe wake uliosomeka:

“Pombe za njaa mbaya sana, unakurupuka kuandika tusi kama hilo kwa mtu ambaye alishakuwa mpenzi wako, kama siyo kukosa akili ni nini?”

 

Chanzo cha tusi hilo kwa mujibu wa ukurasa wa Instagram wa Wolper kinaonesha kuwa msanii huyo wa filamu alichukizwa na mmoja wa watu waliokometi kwenye posti yake ya kunadi ufunguzi wa duka lake jipya kwamba mtaji wa shilingi milioni 30 wa duka hilo alipewa na Harmo.

 

Baada ya madai hayo Wolper alijivua heshima na kuandika tusi zito huku akikumbushia kwamba hata alipokuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmo yeye ndiyo alikuwa “baba lao”.

 

Endapo Harmo atatimiza azma yake ya kumfikisha Wolper kwa pilato kwa ajili ya kutafuta haki na heshima yake basi msanii huyo atashtakiwa kwa makosa ya mtandao na kutumia lugha ya matusi.

Iwapo msanii huyo atatiwa hatiani naweza kuhukumiwa kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kwenda jela miezi sita au vyote kwa pamoja.

STORI: MWANDISHI WETU

Leave A Reply