The House of Favourite Newspapers

Harmonize: Nilijisikia Vibaya Kiba Kukataa Urafiki

0

WIKIENDI iliyopita, Harmonize au Konde Boy Mjeshi alikuwa akizindua albam yake ya High School. Kabla ya uzinduzi huo, Harmonize alipata wasaa wa kuhojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar ambapo alizungumzia mambo mbalimbali.

 

Miongoni mwa mambo hayo ni ile kauli ya msanii mwenzake, King Kiba kukataa kuwa hana urafiki nay eye.

 

Harmonize anasema kuwa, alijisikia vibaya mno mara baada ya kuona video ya mahojiano ya King wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya ambapo alikataa kuwa na urafiki naye baada ya kuulizwa kama ana ukaribu naye.

 

“Kiukweli nilivyoona ile intavyu nilijisikia vibaya kwa mara ya kwanza nikaona inakuwaje hii na huyu ni msanii mwenzangu, tena wote ni Watanzania, lakini mimi mara zote huwa naheshimu maamuzi ya mtu. Na mimi pia ndiyo niliyemwambia tupige picha ya pamoja na nikaiposti baada ya kufahamu kuwa ana shoo Mwanza tulipokutana kwenye ndege,” anasema Harmonize.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply