The House of Favourite Newspapers

Kolabo ya Harmonize & 20 Percent Yanukia

0

HATIMAYE ahadi ya Supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize ‘Teacher Konde’ ya kuingia studio na kufanya kolabo na msanii nguli wa Bongo Fleva, 20 Percent pindi tu akitua kwenye ardhi ya Tanzania toka nchini Marekani imepokelewa kwa mikono miwili na mkali huyo wa zamani.

 

20 Percent ametumia insta story yake kumjibu Harmonize kuwa “Promise is like a debt” (ahadi ni kama deni) kwa maana yupo tayari hivyo Harmonize atimize alichokiahidi.

 

20 Percent ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Kili Music Awards 2010, aliwahi kutamba na ngoma kama Maisha ya Bongo, Mama Neema, Money Money, Tamaa Mbaya na nyingine kibao.

 

Haya yanajiri baada ya usiku wa kuamkia leo kuwa mrefu sana kwa Harmonize alionekana akiburudika na midundo ya 20 Percent na kupelekea kutoa ahadi ya kufanya nae kolabo, sambamba na kueleza kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

 

Leave A Reply