The House of Favourite Newspapers

Shilole, Esha Kimeumana

0

MSANII wa muziki wa Bongo Flava na mmiliki wa mgahawa wa Shishi Food, Shilole amedai kwamba hawezi kujibizana na mtu mitandaoni kiholela holela tu maana yeye ni brand kubwa kwa sasa.

 

Shilole ametoa kauli hiyo kufuatia kilichotokea kwenye Listening Party ya Albamu ya Alikiba ya ONLY ONE KING ya Ocktoba 6, mwaka huu kuonekana Shilole akipewa shavu kubwa zaidi kwenye event hiyo kuliko Esha Buheti ambaye amekuwa akimsapoti Alikiba kwenye kazi zake kwa muda mrefu.

 

Wawili hao wote ni wasanii na wafanyabiashara ya chakula, hivyo inasemekana hicho pia kimechagiza zaidi tofauti baina yao hadi kufikia hatua ya Esha kujitoa kuwa kama shabiki kwa Alikiba.

 

Shishi amedai hawezi bishana na Esha, kwanza hajui kama hilo jambo lina ukweli ndani yake, na kama ni hivyo lazima Esha ajue Event ya Alikiba ilihitaji watu wakubwa, na Alikiba akafanya hivyo kumualika yeye kama msanii mkubwa na kama dada yake, na pia Brand ya Shishi sio ya kujibizana hovyo na watu mitandaoni.

 

Jambo jingine alilolisema Shilole ni kwamba amewazidi followers wote wawili kwenye mitandao ya kijamii, hivyo Shishi ni Brand kubwa Kimataifa.

 

Nini maoni yako?

Leave A Reply