The House of Favourite Newspapers

Video: Rais Magufuli Akipokea Ndege Iliyokamatwa Canada

0

Rais Dk. John Magufuli leo Jumamosi Desemba 14, anaongoza Watanzania kuipokea ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 katika Uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kuachiwa nchini Canada iliposhikiliwa baada ya kutengenezwa.

 

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwemo Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe, Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Palamagamba Kabudi na viongozi wengine pamoja na mamia ya wananchi.

 

Rais Dkt Magufuli amesema wajumbe wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa na mkutano mkoani Mwanza, na wanatarajia kurudi Dar es Salaam, wapelekwe bure na ndege mpya inayotarajiwa kuwasili leo. Amesema hata wale wasioishi Dar es Salaam lakini wanataka kwenda kutembea waende.

 

“Ndege hii kuletwa na marubani Watanzania tumeokoa Dola 40,000 ambazo tulitakiwa kuwalipa marubani wa Canada, Waziri naomba vijana wakifika uwape shukrani zangu kila mmoja umpatie Sh milioni mbili kama shukrani kwa uzalendo wao.

 

“Hii ndege tunayoipokea leo ilitakiwa kufika hapa nchini tangu Novemba lakini kutoka na baadhi ya watu kufungua kesi ikashikiliwa lakini kutokana na juhudi zilizofanywa hatimaye leo tutaipokea hapa Mwanza,” amesema Magufuli.

 

Aidha, Magufuli amesema, jitihada za kuongeza usafiri wa anga na viwanja vyake pia vinasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambapo mpaka sasa kuna jumla ya marubani zaidi ya 90, wahandisi wa ndege 120 na wahudumu wa ndege wengi tu.

 

Ameongeza kuwa, Serikali ina mpango wa kununua ndege ya mizigo ili kuwarahisishia wafanyabiashara wa nyama, maua, matunda wawe wanasafirisha kwa haraka na kufanya biashara zao kwa haraka.

 

Leave A Reply