The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yataifisha Tanzanite Simanjiro

0

JULAI 29, 2020, MAHAKAMA  mkoani Manyara, Julai 29, 2020,  imeyataifisha madini ya Tanzanite gramu 132.64 yenye thamani ya shilingi milioni 18,446,894.14 yaliyokutwa kwa mfanyabiashara wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, kinyume na sheria.

 

Mfanyabiashara huyo wa madini ya Tanzanite wilayani humo, Lucas Liaseki, amekamatwa na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara mbele ya hakimu mkazi, Simon Kobelo, baada ya kujaribu kutorosha madini ya Tanzanite katika geti la ukaguzi wa madini hayo Mirerani.

 

Wakili wa serikali mwandamizi ambaye pia ni mkuu wa mashtaka mkoa wa Manyara, Mutalemwa Kishenyi, amesema mfanyabishara huyo alikamatwa kwa kosa la kutokuwa na kibali cha ambapo serikali imeyataifisha.

 

Aidha, amesema mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi 12 na kumuamuru asifanye kosa lolote kwa kipindi hicho.

Leave A Reply