The House of Favourite Newspapers

Maumivu ya Harmo Yamtesa Kajala

0

UBUYU wa ndani kabisa unadai kwamba; kumbe maumivu ya kutendwa na staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ bado yanamtesa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja.

 

Miezi michache baada ya kufaidi penzi lao, Kajala alifikia hatua ya kumtupia virago Harmonize au Harmo baada ya jamaa huyo kutuhumiwa kumtongoza binti wa mwanamama huyo, Paula Paul almaarufu Paula Kajala.

 

Watu wa karibu wa Kajala wananyetisha kwamba, kama kuna mtu anamfuatilia mwanamama huyo atagundua kuwa, bado kuna vitu vinamtesa kwenye mtima wake kutokana na namna alivyojitoa kwa Harmo kwa moyo wake wote.

 

“Unajua Kajala alimpenda sana Konde Boy (Harmo) na alijua amepata mtu wa kutulia naye na kujenga maisha, lakini mambo hayakwenda kama alivyopanga hivyo ana msongo kama wote,” amedai mmoja wa watu wake wa karibu na kuongeza;

 

“Kama mtu anataka kuamini, aangalie captions (maelezo ya picha) anazoweka kwenye kurasa zake za kijamii, utagundua bado penzi la Harmonize linamtesa.”

 

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limetembelea kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kukutana na ‘captions’ hizo ambazo zinawafanya wafuasi wake wampe pole na kumshauri kujitahi kumsahau jamaa huyo.

 

“Never put the key to your happiness in somebody else’s pocket…(kamwe usiweke ufunguo wa furaha yako kwenye mfuko wa mtu mwingine…)

 

“Get calm and the right answers come…(kaa kimya na majibu sahihi yatakuja…)

“Whatever you do… Do it with all your heart…(chochote unachofanya, fanya kwa moyo wako wote…)  

 

“You don’t always have to tell your side of the story…Time will…(Mara zote huhitaji kueleza upande wa pili wa stori yako… Muda utasema…)

 

“Don’t lose your soul for people who don’t have one….(usipoteze moyo wako kwa mtu asiyejali…”

“You know the truth hurts, but secret kills…(Unajua ukweli unauma, lakini siri inaua…)”

 

Hizo ni baadhi ya jumbe za Kajala zinazotafsiriwa kuwa bado ana maumivu ya penzi la Harmo.

Katika mahojiano maalum na gazeti pacha la hili, IJUMAA, Kajala alisema kuwa, hataki kuulizwa au kumsikia jamaa huyo.

“Sitaki kusikia mambo hayo kwa sasa, ningeachwa kwanza,” alisema Kajala.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply