The House of Favourite Newspapers

Mbowe: Kupona kwa Tundu Lissu ni Mpango wa Mungu

0
Tundu Lissu na Freeman Mbowe.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amefunguka kuhusu hali ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye yupo nchini Nairobi kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Dodoma.

Mbowe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameeleza kuwa kupona kwa Lissu ni mpango wa Mungu pekee!

Kupona kwa Mhe. Lissu ni mpango wa Mungu, nawaomba Watanzania wenzetu waendelee kumuombea kwa Mungu pamoja na kuchangia gharama za matibabu, kwa kuwa gharama zake ni kubwa ambazo chama pekee hakiwezi kuzimudu bila ya misaada kutoka kwa watu mbalimbali.

“Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya.

“Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika.

UPINZANI NI KAZI NGUMU

“Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.

“Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.

“Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatenegeneza hasira kubwa ndani ya jamii,” ameandika Mbowe.

 

Aliyenusurika Ajali Iliyoua Watanzania 13 Uganda Afunguka Ilivyokuwa

Leave A Reply